Monday, March 30, 2015

MICHUANO YA KUFUZU ULAYA YAZIDI KUNOGA.

HEKAHEKA ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Ulaya inayotarajiwa kufanyika mwakani iliendelea tena jana kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwnaja tofauti. Katika mchezo hiyo Ureno waliokuwa wenyeji walifanikiwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kuichapa Serbia kwa mabao 2-1. Kwa upande mwingine Hungary wao walishindwa kuutumia uwanja wao wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Ugiriki katika mchezo wa kundi F huku Ireland ya Kaskazini ikiichapa Finland kwa mabao 2-1 katika mchezo mwingine wa kundi hilo. Kwa upande wa kundi D mabingwa wa dunia Ujerumani waliionyesha kazi Georgia kwa kuichapa mabao 2-0, Jamhuri ya Ireland ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Poland huku Scotland wakiwafundisha soka Gibraltar kwa kuwachapa mabao 6-1.

No comments:

Post a Comment