NAHODHA wa Bayern Munich, Philipp Lahm ana uhakika kuwa kikosi chao kinaweza kushinda mataji matatu kwa mkupuo msimu huu. Lahm ambaye alikuwa akijiuguza majeraha ya kifundo cha mguu alicheza mechi yake ya kwanza jana toka Novemba wakati alipotokea benchi katika ushindi wa mabao 4-0 iliyopata Bayern dhidi ya Werder Bremen. Nyota huyo ambaye amestaafu soka la kimataifa amesema anajisikia furaha kurejea wakati kikosi chake kikiwa imara na ana matumaini wataendelea hivyo mpaka mwishoni mwa msimu wakipigania mataji ya Bundesliga, Ligi ya Mabingwa Ulaya Kombe la Ujerumani. Lahm aliendelea kudai kuwa baada ya kupita kipindi kirefu akiwa akiwa nje anadhani amerejea kwa wakati muafaka ili kukiongezea nguvu kikosi chao kiweze kuendelea kufanya vyema. Ushindi wa jana umeifanya Bayern kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Bundesliga kwa tofauti ya alama 14.
No comments:
Post a Comment