Thursday, March 12, 2015

LIGI KUU HATARINI KUKOSA MWAKILISHI KATIKA ROBO FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE.

KUTOLEWA kwa Chelsea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushindwa kwa sheria ya bao la ugenini kwa Paris Saint Germain, kunaweza kudhihirisha kuwa Ligi Kuu ya Uingereza sio bora duniani kama watu wengi wanavyodhani. Mwezi mmoja baada ya kusaini mkataba mnono wa paundi milioni 5.1 wa haki za matangazo ya moja kwa moja, kuna uwezekano mkubwa kwa mara ya pili katika kipindi cha misimu mitatu timu za Uingereza zikashindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Timu za Uingereza zilizobakia katika michuano hiyo hali zao inaonyesha kuwa dhofule kutokana na kibarua kigumu wanachokabiliwa nacho huko mbele. Arsenal ambao wanakwenda nchini Italia kucheza mchezo wa mkondo wa pili tayari wako numa kwa mabao 3-1 waliyofungwa na AC Milan katika mchezo wa mkondo wa kwanza huku Manchester City nao pia wakiwa nyuma kwa mabao 2-1 dhidi ya Barcelona wakati wakisafiri kwenda Camp Nou. Kwa upande wa michuano ya Europa League nako sio shwari kwani Uingereza inawakilishwa na Everton pekee katika hatua ya timu 16 bora.

No comments:

Post a Comment