MSHAMBULIAJI wa zamani wa Real Madrid, Raul amesema kikosi cha sasa kina ubora wa kuweza kurejea katika kiwango chao baada ya kupita kipindi cha mpito cha kucheza chini ya kiwango. Madrid walijikuta wakizomewa wakati wakitoka uwanjani katikati ya wiki iliyopita baada ya kutandikwa mabao 4-3 dhidi ya Schalke katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo hata hivyo walizonga mbele kwa jumla ya mabao 5-4. Matokeo hayo yakafuatiwa na sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya Villarreal huku wakichapwa na Athletic Bilbao kwa bao 1-0 na kupoteza nafasi yao ya kuongoza La Liga. Pamoja na hayo Raul bado ana imani kuwa timu inaweza kurejea katika ubora wake na kuendelea kushinda michezo yake kama ilivyokuwa miezi michache nyuma. Raul mwenye umri wa miaka 37, amewahi kushinda mataji sita ya La Liga na matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka 15 alichoichezea Madrid na sasa anacheza katika timu ya New York Cosmos ya Marekani.
No comments:
Post a Comment