MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini hadhani kama mbio za kutetea taji lao la Ligi Kuu zimekwisha baada ya kukubalia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Burnley jana. Kipigo hicho ni pigo kubwa kwa City ambao wanafukuzia tajila taji katika kipindi cha misimu minne lakini bado wamebaki katika nafasi ya pili katika msimamo wakiwa nyuma ya Chelsea kwa alama 58 huku kukiwa kumebaki michezo tisa kabla ya msimu kumalizika. Akihojiwa baada ya mchezo huo Pellegrini amesema wakati ukiwa na nafasi kimahesabu hakuna shaka kuwa una nafasi ya kunyakuwa taji. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa bado ni mapema sana kuwaondoa katika mbio hizo kwasababu kimahesabu bado wana nafasi ya kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment