MENEJA wa Manchester United, Luis van Gaal anadhani bado anaungwa mkono na wachezaji wake lakini amedai anaweza kuachia ngazi kama kikosi chake kitapoteza imani katika mipango yake. Kumekuwa na tetesi za mgomo kwa baadhi ya wachezaji wa United huku nyota wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi Willem van Hanegem akimtuhumu Van Gaal kwa kutowatendea visivyo Ryan Giggs, Radamel Falcao na Angel Di Maria. Hata hivyo tetesi hizo zimekanushwa vikali na Van Gaal aliyedai kuwa wana maelewano mazuri na wachezaji wake na wanaunga mkono mbinu zake. Van Gaal aliendelea kudai kuwa kama ataona mbinu zake hazieleweki miongoni mwa wachezaji atakuwa wa kwanza kuachia ngazi na kupisha wengine.
No comments:
Post a Comment