MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi ametania kuwa ghafla ametoka kucheza hovyo mpaka kurejea katika ubora wake baada ya kuonyesha kiwango murua katika mchezo wao wa maruadiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alitengeneza bao pekee lililofungwa na Ivan Rakitic katika mchezo huo na kuwaondosha mashindanoni mabingwa hao wa Uingereza kwa jumla ya mabao 3-1 katika michezo miwili waliyokutana. Messi amemmwagia sifa kedekede mlinga mlango wa City Joe Hart kwa kazi kubwa aliyofanya katika mchezo huo lakini alipuuza taarifa kuwa hivi sasa amejerea katika ubora wake. Akihojiwa Messi amesema katika siku sio nyingi watu wengi walikuwa wakihoji kuhusu kiwango chake na kudai kuwa haiwezekano abadilike ghfla namna hiyo kama watu wengi wanavyodhani. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa walifanya kila wanaloweza kuhakikisha wanafunga mabao mengi kwenye mchezo huo lakini Hart alikuwa kikwazo kikubwa kwao na anampongeza kwa juhudi zake. Messi amesema sasa anadhani wako katika kiwango kizuri kuelekea katika mchezo wao wa El Classico ambao utawakutanisha na mahasimu wao Real Madrid Jumapili hii.
No comments:
Post a Comment