CHAMA cha Soka cha Misri-EFA kimetangaza jana kumteua Hector Cuper kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo. EFA imekuwa ikitafuta kocha mpya baada ya kumtimua Shawky Gharib ambaye alishindwa kuiwezesha Misri kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika iliyopita. Kabla ya kumtangaza Cuper, EFA iliwafanyia usaili makocha wengine kadhaa akiwemo kocha wa Ivory Coast Herve Renard na Alain Giresse. Kibarua cha kwanza cha Cuper ambaye ni raia wa Argentina, itakuwa ni kuhakikisha Misri inafuzu michuano ya Afcon ya mwaka 2017. Cuper mwenye umri wa miaka 59 amewahi kuzinoa klabu za Mallorca, Valencia, Internazionale, Real Betis, Parma na timu ya taifa ya Georgia.

No comments:
Post a Comment