MSHAMBULIAJI nyota wa Juventus, Carlos Tevez amedai kugadhabishwa kama ilivyo kwa meneja wake Massimiliano Allegri baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya AS Roma jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina ndiye aliyefunga bao la kuongoza katika dakika ya 64 ya mchezo lakini walishindwa kulinda bao hilo baada ya Seydou Keita kusawazisha katika dakika za majeruhi. Akihojiwa Tevez amesema kocha wao ana haki ya kugadhabika kutokana na kushindwa kwao kulinda bao katika mchezo huo muhimu. Tevez amesema walicheza vyema katika dakika 70 za mchezo lakini walijisahau kwenye dakika 20 za mwisho.

No comments:
Post a Comment