RAIS wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola, Prince Imran amesema michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 kufanyika Desemba itakuwa na faida kwa michuano hiyo. Kikosi kazi cha Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kimependekeza michuano hiyo ambayo itafanyika Qatar kufanyika katika miezi ya Nivemba na Desemba. Kuamishwa kwa michuano hiyo kutoka kwa miezi yake iliyozoeleka ya Juni na Julai kunaicha michuano ya Jumuiya ya Madola kuwa pekee itakayofanyika katika majira ya kiangazi mwaka huo. Akihojiwa Prince Imran amesema hiyo taarifa njema kwao na nafasi kubwa kwani hakutakuwa na michuano mingine yeyote zaidi ya Jumuiya ya Madola katika kipindi hicho. Mji wa Durban wa Afrika Kusini umebakia kuwa mji pekee unagombea nafasi ya kuandaa michuano hiyo baada ya mji wa Edmonton wa Canada kujitoa.

No comments:
Post a Comment