KLABU ya Tottenham Hotspurs imetangaza kuwa nahodha wake wa zamani Dave Mackay amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80. Nguli huyo wa zamani wa kimataifa wa Scotland amewahi kushinda mataji mawili akiwa na Spurs mwaka 1961 huku pia akiingoza Derby County kushinda taji la ligi akiwa kama meneja. Katika taarifa yake Spurs imeeleza kusikitishwa kwake kuondokewa na mmoja kati ya wachezaji waliopa mafanikio timu hiyo enzi hizo. Spurs imemuelezea Mackay kama mchezaji aliyekuwa na maarifa ya hali ya juu na mchezaji aliyekamilika pindi anapokuwa uwanjani.

No comments:
Post a Comment