Tuesday, March 3, 2015

FA YATENGUA KADI YA WES BROWN.

CHAMA cha Soka cha Uingereza-FA kimetengua kadi nyekundu aliyopewa beki wa Sunderland Wes Brown wakati amchezo dhidi ya Manchester United uliochezwa Jumamosi iliyopita. Brown alipewa kadi hiyo pamoja na picha za video kuonyesha kuwa beki mwenzake John O’Shea ndio aliyemfanyia madhambi mshambuliaji wa United Radamel Falcao. Hata hivyo pamoja na kufutwa kwa kadi hiyo, O Shea naye hataadhibiwa hivyo kuwafanya kuwepo katika mchezo leo wa Ligi Kuu dhidi ya Hull City. Meneja wa Sunderland Gus Poyet ameupongeza uamuzi huyo kuwa wa kiungwana haswa baada ya kuona kuwa walifanya makosa.

No comments:

Post a Comment