Friday, March 6, 2015

NASRI ATAMANI KUFUATA NYAYO ZA LAMPARD.

KIUNGO mahiri Samir Nasri amebainisha kuwa angependa kufuata nyayo za mchezaji mwenzake wa Manchester City Frank Lampard kwa kujiunga klabu za Ligi Kuu nchini Marekani-MLS. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ana miaka saba katika Ligi kuu nchini Uingereza akiwa ameshinda mataji mawili ya ligi na moja la Kombe la Ligi toka ajiunge na City akitokea Arsenal katika majira ya kiangazi mwaka 2011. Akihojiwa Nasri amesema ingawa anapenda kuitumikia klabu yake ya utotoni ya Marseille wakati akirejea nyumbani kwao Ufaransa lakini pia ana ndoto za kwenda kucheza soka marekani. Nasri amesema kikubwa kinachomfanya avutiwe kwenda kucheza Marekani ni aina ya maisha yaliyopo huko. Akiulizwa klabu ambayo angependa kuichezea Marekani, Nasri amesema anapenda kucheza katika klabu yeyote inayotoka katika miji mikubwa.

No comments:

Post a Comment