Friday, March 6, 2015

WENGER AMKINGIA KIFUA OZIL BAADA YA KUKOSOLEWA NA SCHOLES.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amemkingia kifua Mesut Ozil baada ya kukosolewa na Paul Scholes akisisitiza kuwa ni mchezaji anayejituma na nyota huyo wa zamani wa Manchester United angefurajia kucheza naye. Kauli hiyo ya Wenger imekuja kufuatia Scholes kumkosoa Ozil akidai kuwa hana morali ya kushinda taji la Ligi Kuu kutokana na kiwango duni anachoonyesha. Hata hivyo Wenger amepingana vikali na kauli hiyo ya Scholes akidai hakumtendea haki kwani kama angekuwa anacheza naye lazima angemfurahia. Wenger amesema Ozil ana ubora unaotakiwa na anafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha Arsenal inapata matokeo mazuri. Wenger aliendelea kutamba kuwa wanatakwenda kucheza na Manchester United wakihitaji kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la FA ili waweze kusonga mbele na kwenda kutetea taji lao.

No comments:

Post a Comment