Friday, March 20, 2015

ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE: MADRID KUKWAANA NA ATLETICO, BARCELONA NA PSG.

MABINGWA watetezi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid wamepangwa kucheza na mahasimu wao wa jiji Atletico Madrid katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Mchezo huo utakuwa kama marudio ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo uliokutanisha timu hizo msimu uliopita ambapo Real Madrid ilishinda kwa kuinyuka Atletico kwa mabao 4-1 na kunyakuwa taji lao la 10. Katika mechi zingine zilizopangwa Paris Saint-Germain wamepangwa kukwaana na Barcelona wakati mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakipangiwa kucheza na FC Porto huku Juventus wao wakianzia nyumbani kupepetana na AS Monaco. Fainali ya michuano hiyo kwa mwaka huu inatarajiwa kufanyika Juni 6 katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin, Ujerumani

No comments:

Post a Comment