Sunday, March 22, 2015

USHINDI WAMPA JEURI PELLEGRINI.

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amesema huwa anafuatilia matokeo ya timu yake pekee baada ya kufanikiwa kuifunga West Bromwich Albion na kuongeza msukumo wa vinara wa Ligi Kuu Chelsea. Ushindi wa mabao 3-0 waliopata katika mchezo wa jana umepunguza pengo la alama kufikia tatu kati yao na Chelsea ingawa wapinzani wao hao bado walikuwa na mchezo mkononi. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Pellegrini amesema jambo la muhimu ni kuhakikisha wanashinda mechi nane zilizobakia na hana mpango wa kufuatilia matokeo ya wengine kwasasa. Pellegrini aliendelea kudai kuwa hataweza kutazama mchezo kati ya Chelsea na Hull City leo na badala yake atafuatilia mchezo kati ya Liverpool na Manchester United ambao watacheza na City mchezo ujao.

No comments:

Post a Comment