Sunday, March 22, 2015

MAN UNITED YAICHAPA LIVERPOOL NYUMBANI KWAO HUKU GERRARD AKIPEWA KADI NYEKUNDU.

KLABU ya Manchester United leo imefanikiwa kujiimarisha katika nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu baada ya kuifunga Liverpool mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Anfield. Katika mchezo huo United ndio walitangulia kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Juan Mata katika dakika ya 11 kabla ya kiungo huohuyo kuongeza bao lingine katika dakika ya 59. Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo kwa kumchezea faulo Andre Herrera ikiwa zimepita sekunde 48 toka aingie uwanjani akitokea benchi akichukua nafasi ya Adam Lallana. Bao la kufutia machozi la Liverpool katika mchezo huo lilifungwa na Daniel Sturridge huku Wayne Rooney akikosa penati katika dakika za mejeruhi ambayo iliokolewa na Mignolet.

No comments:

Post a Comment