Tuesday, March 24, 2015

STURRIDGE PANCHA TENA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uingereza Daniel Sturridge anatarajiwa kuikosa michezo ya nchi yake dhidi ya Lithuania na Italia baada ya kupata majeruhi tena. Nyota huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 25 alipata majeraha ya nyonga katika mchezo dhidi ya Manchester United uliofanyika Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Anfield. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa Chama cha Soka cha nchi hiyo-FA, kilithibitisha taarifa hiyo na kudai kuwa nyota huyo amerejea katika klabu yake jana jioni. Hatua hiyo inafuatia baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari kung’amua kuwa hataweza kulitumikia taifa lake katika michezo hiyo. Kukosekana kwa Sturridge kunaweza kuwa nafasi kwa Harry Kane kupata nafasi yake ya kwanza kucheza katika kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa ya nchi hiyo. Mbali na Sturridge lakini pia mchezaji mwenzake wa Liverpool Adam Lallana naye alirudishwa baada ya kuwa majeruhi na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo wa Tottenham Hotspurs Ryan Mason.

No comments:

Post a Comment