MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Luis Suarez kwa mara nyingine amevishambulia vyombo vya habari vya Uingereza akidai kuwa amevikumbuka kwa jinsi walivyokuwa wakimfuatilia. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 28 aliondoka Liverpool kwenda Barcelona katika majira ya kiangazi mwaka jana lakini bado ameendelea kuwa na mahusiano mabovu na vyombo vya habari vya Uingereza. Baada ya vyombo vya habari nchini humo kudai kuwa Suarez alionekana kama alitaka kumng’ata Martin Demichelis katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi uliopita, nyota huyo amesema ameshachoshwa na kuzushiwa. Akihojiwa Suarez amesema hafahamu vyombo vya habari vya Uingereza vinataka nini kwake lakini inaonekana labda wamemkumbuka baada ya kuondoka. Nyota huyo amesema wamekuwa wakimkosoa sana na siku zote wanatafuta vitu vinavyoweza kuvuta hisia za watu.
No comments:
Post a Comment