Friday, March 13, 2015

MANCINI AKATAA KULAUMU WACHEZAJI WAKE BAADA YA KIPIGI KUTOKA WOLFSBURG.

MENEJA wa Inter Milan, Roberto Mancini amekataa kumlaumu Juan Pablo Carrizo kwa kipigo cha mabao 3-1 walichopata dhidi ya Wolfsburg katika michuano ya Europa League. Wolfsburg walitoka nyuma na kupata ushindi huo muhimu jana huku golikipa huyo akionekana kama hakufanya kazi yake yake sawasawa katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza. Pamoja na hayo Mancini alimtetea Carrizo akidai kuwa mabao yasingefungwa kama wasingekuwa wanapoteza mipira kirahisi kwa wapinzani wao. Mancini amesema Carrizo anaweza kuwa alifanya makosa mapema katika kipindi kwanza lakini pia alijitahidi kuokoa michomo mingi katika lango lao.

No comments:

Post a Comment