Friday, March 13, 2015

TANZANIA YAKWEA MPAKA NAFASI YA 100 KATIKA VIWANGO FIFA.

TANZANIA imekwea mpaka nafasi ya 100 katika orodha za ubora wa soka duiani ambazo hutolewa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kila mwezi. Mwezi uliopita Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 107 lakini katika orodha mpya zilizotolewa mwezi huu inaonekana kukwea kwa nafasi saba huku kwa upande wa Afrika wakishikilia nafasi ya 28. Algeria ndio vinara kwa Afrika wakiwa katika nafasi ya 18 wakifuatiwa na mabingwa wa Afrika Ivory Coast ambao wako nafasi ya 20 huku Ghana wao wakiwa nafasi ya tatatu kwa kushika nafasi ya 24. Tunisia yuko katika nafasi ya nne kwa Afrika baada ya kushika nafasi ya 25 duniani wakifuatiwa na Senegal ambao ndio wanafunga tano bora ya Afrika kwa kuwa nafasi ya 36 duniani. Kwa upande wa tano bora duniani hakuna mabadiliko yeyote kwani Ujerumani bado wanaongoza wakifuatiwa na Argentina katika nafasi ya pili, Colombia nafasi ya tatu, Ubelgiji nafasi ya nne na tano bora inafungwa na Uholanzi.

No comments:

Post a Comment