KATIKA habari za tetesi za usajili zilizopamba vichwa habari vya magazeti na mitandao mbalimbali Ulaya ni pamoja na meneja wa Chelsea Jose Mourinho amemuweka katika rada zake beki wa kimataifa wa Ufaransa na Real Madrid Raphael Varane kwa ajili ya kumsajili kiangazi. Mourinho anatarajiwa kupewa kitita cha paundi milioni 75 kwa ajili ya kukisuka kikosi chake baada ya kutolewa katika hatua ya 16 bora katika michuano ya Ligi ya Mabingwa. Chelsea pia imepanga kumuongeza mkataba mpya Mourinho pamoja na kutolewa katika michuano hiyo baada ya mkataba wake wa sasa kubakisha miaka miwili kabla ya kumalizika. Klabu ya Liverpool ina matumaini ya kuanza mazungumzo na beki wa kimataifa wa Brazil Dani Alves mwenye umri wa miaka 31 ambaye anatarajiwa kuondoka Barcelona wakati mkataba wake utakapomaliza katika majira ya kiangazi. Dynamo Kiev ya Ukraine wanataka kumbakisha beki wao Aleksandar Dragovic ambaye anawindwa na klabu ya Arsenal. Southampton inahofia kuja kushindwa kumpa mkataba wa kudumu beki wa Atletico Madrid Toby Alderweireld ambaye yuko kwao kwa mkopo kutokana na beki huyo kutaka kwenda katika klabu nyingine kiangazi. Arsenal wanaweza kumruhusu beki wake Carl Jenkinson mwenye umri wa miaka 23 kujiunga na West Ham United moja kwa moja katika majira ya kiangazi baada ya kutuma ofa ya kumsajili Hector Bellerin mwenye umri wa miaka 19.
No comments:
Post a Comment