GOLIKIPA wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya TP Mazembe Sylvain Gbohouo amesafiri kwenda nchini Qatar kwa ajili ya matibabu ya goti. Gbohouo ndiye aliyekuwa golikipa chaguo la kwanza la Ivory Coast katika michuano ya Mataifa ya Afrika iliyochezwa Januari mwaka huu huko Guinea ya Ikweta ambapo nchi yake ndio iliyoibuka kidedea. Golikipa huyo alikosa mchezo wa fainali dhidi ya Ghana baada ya kupata majeruhi ya goti wakati wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Gbohouo ambaye ametua Mazembe baada ya michuano hiyo ya Afrika bado hajacheza mechi yeyote mpaka sasa. Rais wa Mazembe Moise Katumbi amesema wamemruhusu golikipa kwenda kupatiwa matibabu chini ya usimamizi wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast.
No comments:
Post a Comment