Tuesday, March 24, 2015

UEFA YAZIONYA TIMU KUHUSU WACHEZAJI WAO KUWABUGUDHI WAAMUZI.

KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Gianni Infantino amezionya timu zote zilizotinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuwaonya wachezaji wao kutowabugudhi waamuzi. Infatino pia ameongeza shirikisho hilo halitaunga mkono kutumia picha video ili kugundua makosa ya waamuzi wakati mchezo ukiendelea. Ofisa wa waamuzi wa UEFA Pierluigi Collina alizionya timu za Atletico Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Juventus, Monaco, Paris Saint Germain, Porto na Real Madrid katika kikao walichokutana Ijumaa iliyopita. Kikao hicho kilichofanyika jijini Nyon, Uswisi kimekuja ikiwa imepita siku moja baada ya shirikisho hilo kumfungia mechi tatu beki wa PSG Serge Aurier kwa kutoa maneno ya kashfa kwa mwamuzi katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea. Aurier hakucheza mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 lakini alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook kumponda mwamuzi Bjorn Kuipers kwa kumtoa nje kwa kadi nyekundu Zlatan Ibrahimovic.

No comments:

Post a Comment