Saturday, March 28, 2015

ZAMBIA YAKWEPA ADHABU KIJANJA.

SERIKALI ya Zambia imemlipa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo Dario Bonetti ili kuepusha adhabu ya kufungiwa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA. Bonetti raia wa Ufaransa ambaye amewahi kuinoa Chipolopolo kuanzia Julai mwaka 2010 hado Octoba mwaka 2011 amekuwa akiidai nchi hiyo kiasi ha dola 432,000. Kocha huyo alitimuliwa huku kukiwa kumebaki miezi tisa katika mkataba wake na pamoja na kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2012. Bonetti alipelekea malalamiko yake FIFA kulishitaki Shirikisho la Soka la Zambia na kesi ilikuwa ikitarajiwa kutolewa maamuzi Agosti mwaka huu. Hata hivyo kufuatia Zimbabwe kuenguliwa katika michezo ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 kwa kushindwa kumlipa kocha wao wa zamani Jose Claudinei Georgini kulikwua na hofu kuwa Zambia wangeweza kupata adhabu kama hiyo hivyo kuamua kumlipa kabla.

No comments:

Post a Comment