Saturday, March 28, 2015

URUSI KUISHITAKI MONTENEGRO BAADA YA VURUGU.

SHIRIKISHO la Soka la Urusi-RFU linakusudia kuwasilisha malalamiko yao rasmi Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA baada ya mchezo wao wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani dhidi ya Mintenegro kusitishwa. Mchezo uliochezwa jana huko Podgorica ulianza kwa utata wakati golikipa wa Urusi Igor Akinfeev kupigwa na kitu mfano wa fataki kutokea jukwaani baada ya mchezo kuanza hatua ilipelekea mchezo huo kusimamishwa kwa muda. Mchezo huo uliendelea tena baada ya kusimamishwa kwa zaidi ya nusu saa huku Akinfeev akikimbizwa hospitalia kutokana na tukio hilo. Baada ya Roman Shirokov kuokoa penati kwa Urusi katika dakika ya 66, mchezaji Dmitri Kombarov alionekana kupigwa na kitu kingine kama hicho kutokea jukwaani hatua ambao ilizusha vurugu kali ndani na nje ya uwanja na kupelekea mchezo kusitishwa kabisa. Rais wa RFU Nikolai Tolstoy amekaririwa akidai kuwa hawezi kuwalaumu mashabiki kwa tabia walioonyesha kwani tayari walikuwa wamewaonya maofisa wa UEFA wakati wa tukio la kwanza lakini waliamua mchezo uendelee. Tolstoy amesema kwa maono yake mchezo huo ulitakiwa kusitishwa toka mara ya kwanza na Montenegro kunyang’anywa alama.

No comments:

Post a Comment