Saturday, March 28, 2015

WENGER APISHANA NA WALCOTT.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa majadiliano ya mkataba na Theo Walcott yameanza pamoja na mshambuliaji huyo kudai kuwa bado. Walcott aliandika katika ukurasa wake wa twitter jana kuwa mazungumzo kuhusu mkataba mpya na Arsenal yalikuwa bado kufanyika jambo ambalo linaonekana kuwa na mkanganyiko baada ya Wenger kudai kuwa tayari wameshaanza kuzungumza naye. Akihojiwa Wenger amesema tayari wameshaanza kuzungumza na Walcott kuhusu uwezekano wa kuongeza mkataba mpya nay eye binafsi anataka nyota huyo aendelee kuitumikia timu hiyo. Walcott amekuwa akipambana kurejea katika kikosi cha kwanza cha Gunners toka atoke katika majeruhi yaliyomchukua karibu mwaka mzima kupona.

No comments:

Post a Comment