Saturday, March 28, 2015

JORDI ALBA KUIKOSA UHOLANZI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amethibitisha kuwa Jordi Alba amerejeshwa Barcelona baada ya kupata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya dhidi ya Ukraine jana. Nyota huyo wa zamani wa Valencia alitolewa nje zikiwa zimebaki dakika 11 mchezo huo walioshinda bao 1-0 na nafasi yake kuchukuliwa na Juan Bernat wa Sevilla. Del Bosque tayari amethibtisha kuwa atakosa huduma ya mchezaji huyo katika mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Uholanzi Jumanne ijayo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa tayari madaktari wa Hispania wameshairifu timu yake na wanatarajia kumruhusu kwa ajili ya kwenda kufanyiwa vipimo zaidi.

No comments:

Post a Comment