Saturday, March 28, 2015

HARRY KANE AFURAHIA KUFUNGA BAO KATIKA MCHEZO WAKE WA KWANZA KUICHEZEA UINGEREZA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uingereza, Harry Kane amebainisha kuwa na wakati mzuri baada ya kufanikiwa kufunga bao katika sekunde 80 toka aanze kuitumikia timu yake ya taifa kwa mara ya kwanza wakati walipopata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lithuania jana. Akiwa ameshaifungia klabu yake ya Tottenham Hotspurs mabao 29, Kane alianzia benchi katika mchezo huo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani lakini aliingia katika dakika ya 71 akichukua nafasi ya Raheem Sterling na kufunga bao ndani ya dakika mbili. Akihojiwa Kane mwenye umri wa miaka 21 amesema sio mbaya kwa kuanzia kwani amekuwa akiiota siku hiyo kwa kipindi kirefu na anashukuru amefanikiwa kutimiza nia yake hiyo. Kane aliendelea kudai kuwa kuiwakilisha timu yake kimataifa na kuisaidia kushinda ni jambo linalomfanya kuwa na fahari kubwa.

No comments:

Post a Comment