Thursday, March 26, 2015

DUDEK AMSHAURI SZCZESNY KUONDOKA ARSENAL.

GOLIKIPA wa zamani wa Liverpool, Jerzy Dudek amemtaka Wojciech Szczesny kuondoka Arsenal baada ya kupoteza nafasi yake kama golikipa namba moja kwa David Ospina. Golikipa huyo alipoteza nafasi hiyo Januari mwaka huu baada ya kukutwa akivuta sigara bafuni baada ya klabu hiyo kufungwa na Southampton katika Uwanja wa St Mary. Toka wakati huo Ospina amekuwa akipata nafasi ya kuanza katika kikosi cha Arsenal na Dudek anadhani wakati umefika kwa Szczesny kuondoka Emirates na kwenda kutafuta timu anayoweza kupata nafasi ya kuanza katika majira ya kiangazi. Dudek amesema suala hilo ni muhimu na Szczesny anapswa kulifikiria kwa makini kwani inavyoonekana tayari ameshapoteza nafasi yake Arsenal.

No comments:

Post a Comment