Thursday, March 26, 2015

KHEDIRA ATHIBITISHA KUONDOKA MADRID.

KIUNGO wa klabu ya Real Madrid, Sami Khedira amethibitisha kuondoka katika timu hiyo wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani amecheza mechi zaidi ya 100 za ligi katika kipindi cha miaka mitano alichokuwa Santiago Bernabeu lakini ameshindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba wa sasa. Khedira mwenye umri wa miaka 27 amesema anataka kutafuta changamoto mpya baada ya kupoteza nafasi yake kwa nyota wengine wa Madrid kama Toni Kroos na Luka Modric lakini amesisitiza bado hajaamua aelekee wapi msimu ujao. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa hajafikia makubaliano na klabu yeyote mpaka sasa, kitu pekee anachofahamu ni kuwa hatakuwa na Madrid msimu ujao kwasababu ya kutafuta changamoto mpya.

No comments:

Post a Comment