Thursday, March 26, 2015

PELE ATAMBA KUWA HATA NEYMAR HAWEZI KUMFIKIA.

NGULI wa soka wa Brazil, Pele amesisitiza kuwa hata Neymar hawezi kufikia ubora wake wakati alipokuwa akisakata kabumbu. Nguli huyo ambaye amewahi kushinda mataji matatu ya Kombe la Dunia akiwa na Brazil na kufunga mabao zaidi ya 1,000 enzi zake, ameshwaona wachezaji kadhaa ambao walikuwa wkaipigania kufikia rekodi yake toka astaafu. Mojawapo ya wachezaji hao ni Ronaldo ambaye amefunga mabao 62 katika mechi za kimataifa na Romario ambaye alikaririwa mapema mwezi huu kuwa Neymar anaweza kuipita idadi ya mabao 77 aliyofunga Pele kwa Brazil. Akiulizwa kama anadhani Neymar anaweza kuchukua nafasi yake kama mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika soka la Brazil, Pele amesema hadhani kama hilo linawezekana. Pele alifafanua kuwa haoni kama litawezekana kuwa na mfalme mpya au Pele mpya kwasababu mama yake na baba yake tayari walishafunga kizazi zamani.

No comments:

Post a Comment