Thursday, March 26, 2015

ANDERSON KUENDELEA KUBAKIA LAZIO - WAKALA.

WAKALA wa mshambuliaji Felipe Anderson amesisitiza kuwa mteja wake amefurahi kukataa kwenda kwenye klabu zinazoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kubakia Lazio msimu huu baada ya kusaini mkataba mpya. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye amefunga mabao 10 na kutoa pasi za mwisho nane katika mechi 25 alizoichezea Lazio msimu huu amekuwa akihusishwa kuwindwa na vilabu mbalimbali vikiwemo Manchester United na Chelsea. Lakini wakala wa mchezaji huyo Stefano Castagna amesema Lazio haitapata tabu kumbakisha nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2020, kwani anafurahia maisha ya Rome. Castagna amesema mteja wake hana mpango wowote wa kuondoka majira ya kiangazi kwani anafurahi kuitumikia klabu hiyo na anapenda kujiimarisha zaidi akiwa hapo.

No comments:

Post a Comment