Thursday, April 2, 2015

ALLEGRI AWASAMEHE MASHABIKI WA JUVENTUS WALIODHARAU UWEZO WAKE.

MENEJA wa Juventus, Massimiliano Allegri amesema amewasamehe mashabiki waliomponda wakati alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Allegri mwenye umri wa miaka 47 alichukua mikoba ya kuinoa Juventus kiangazi mwaka jana, akirithi kikosi ambacho kilifanikiwa kushinda mataji matatu mfululizo ya Serie A chini ya kocha aliyeondoka Antonio Conte. Hata hivyo, Allegri ambaye alikuwa ametimuliwa na mahasimu wakubwa wa Juventus klabu ya AC Milan alishindwa kuwa kipenzi cha mashabiki jijini Turin kutokana na mahali alipotokea. Pamoja na hayo Juventus sasa wako kileleni mwa msimamo wa Serie A kwa tofauti ya alama 14, wakati kocha huyo pia ameiongoza kufika robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na nusu fainali ya Kombe la Mfalme. Matokeo hayo yanamfanya kocha huyo kugeuka na kuwa kipenzi cha mashabiki wale wale waliokuwa wakimponda nay eye mwenyewe anadai kuwa tayari alishawasamehe kwa kukosoa uwezo huko nyuma. Allegri amesema kusamehe ni jambo la haki kufanya kwasababu nadhani wasiwasi wa mashabiki waliokuwa nao wakati akiteuliwa Julai 16 ulikuwa wa kawaida.

No comments:

Post a Comment