Thursday, April 2, 2015

BAYERN KUKOSA HUDUMA YA ALABA KWA WIKI SABA.

KLABU ya Bayern Munich imetangaza kuwa beki wao wa kushoto wa kimataifa wa Austria David Alaba anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki saba baada ya kuumia goti wakati akiitumikia nchi yake. Alaba ambaye pia anaweza kucheza nafasi ya kiungo alipata majeruhi hayo katika goti lake la kushoto katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao Austria ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Bosnia-Herzegovina Juzi. Hata hivyo, Alaba mwenye umri wa miaka 22 amesema ana matumaini ya kurejea uwanjani kabla ya mchezo wao wa mwisho wa msimu wa Bundesliga dhidi ya Mainz ambao umepangwa kuchezwa Mei 23, wiki saba na nusu kutoka sasa. Alaba aliuambia mtandao wa Bayern kuwa majeruhi hayo yamemsononesha lakini amejiwekea lengo moja kubwa nao ni kurejea uwanjani kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa ligi. Barcelona bdo wapo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ambayo fainali yake itachezwa Juni 6 mwaka huu jijini Berlin.

No comments:

Post a Comment