Thursday, April 2, 2015

MESSI ATAKUWA FITI KUIVAA CELTA VIGO - PIQUE.

BEKI wa kati wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique amesema anatarajia Lionel Messi kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa La Liga dhidi ya Celta Vigo Jumapili hii pamoja na wasiwasi wa kuwa majeruhi. Akihojiwa Pique amesema alizungumza na Messi na ana uhakika atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo ambao utachezwa katika Uwanja wa Balaidos unaomilikiwa na Ceta Vigo. Beki huyo aliendelea kudai kuwa mwisho wa siku madaktari ndio watakaoamua kuhusiana na suala hilo lakini anafikiri ataweza kucheza. Katika mchezo uliopita Barcelona walifanikiwa kuwafunga mahasimu wao Real Madrid kwa mabao 2-1 na kutanua pengo la alama kufikia nne huku kukiwa kumebaki michezo 10 kabla ya msimu kumalizika.

No comments:

Post a Comment