MKURUGENZI wa michezo wa Juventus, Pavel Nedved amekiri Barcelona na kila klabu nyingine kubwa Ulaya wanataka kumsajili kiungo Paul Pogba lakini akatahadharisha kuwa nyota huyo atabakia chini ya mkataba na mabingwa hao wa Italia. Toka ajiunge na Juventus kwa uhamisho huru akitokea Manchester United mwaka 2012, Pogba amejiimarisha na kuwa mchezaji tegemeo wa timu hiyo huku akikadiriwa kufikia thamani ya euro milioni 100. Real Madrid na Paris Saint-Germain zimekuwa zikimfukuzia nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa muda lakini Barcelona sasa ndio wanatajwa kuwa na nafasi ya kumsajili. Akihojiwa Nedved amesema anajua Barcelona na vilabu vingine vikubwa vinamtaka lakini kwasasa bado ana mkataba na Juventus ambao unamalizika mwaka 2019. Kwasasa Pogba yuko nje ya uwanja akiuguza majeruhi ya msuli wa paja ambapo anatarajiwa kurejea Mei mwaka huu.

No comments:
Post a Comment