Friday, April 17, 2015

DAKTARI WA BAYERN AJIUZULU KUFUATIA KIPIGO.

DAKTARI wa klabu ya Bayern Munich, Hans-Wilhelm Muller-Wolhfahrt amejiuzulu baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 38, akidai kuwa kitengo cha afya kinapaswa kulaumiwa kutokana na kipigo walichopata kutoka kwa FC Porto katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bayern iliwakosa nyota wake kadhaa muhimu katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ambao walichapwa mabao 3-1. Muller-Wohlfahrt mwenye umri wa miaka 72 amesema kutokana na sababu zisizoelezeka ni kitengo cha afya ndio kinapaswa kulaumiwa kwa matokeo hayo. Daktari huyo mkongwe amesema uhahusiano baina ya kitengo hicho na wachezaji umekuwa na mpasuko. Mawinga Franck Riberyn na Arjen Robben, kiungo Bastian Schweinsteiger na beki David Alaba wote walikosa mchezo huo wa Jumanne kwasababu ya majeruhi. Muller-Wohlfahrt ambaye pia amekuwa akifanya kazi kama daktari wa timu ya taifa ya Ujerumani amekuwa akiwatibu wanamichezo maarufu akiwemo bingwa mara sita wa michuano ya olimpiki Usain Bolt kutoka Jamaica.

No comments:

Post a Comment