Wednesday, April 8, 2015

GABON NDIO MWENYE MPYA WA AFCON MWAKA 2017.

SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limeichagua Gabon kuwa mwenyeji mpya wa michuano ya Mataifa ya Afrik-Afcon mwaka 2017. Gabon ambao waliakuwa wenyeji wenza wa michuano hiyo mwaka 2012 walimeshinda nafasi hiyo na kuzipiku nchi za Algeria na Ghana ambazo nazo zilikuwa zikiiwania. Hiyo inakuwa mara ya pili kwa nchi hiyo iliyopo pwani ya magharini mwa Afrika kushinda nafasi hiyo baada ya kuagwana majukumu na Guinea ya Ikweta mwaka 2012. Wenyeji halisi Libya walijitoa mwaka jana kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo toka kuondolewa kwa utawala wa rais Muamar Gadaffi mwaka 2011. Gabon itatumia viwnaja vinne kwa ajili ya timu 16 zitakazoshiriki michuano hiyo ambavyo ni Libreville na Franceville vilivyotumiwa mwaka 2012 huku Port Gentil na Oyem viwnaja vyake vikitarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 14 ijayo.

No comments:

Post a Comment