Wednesday, April 8, 2015

TANZANIA YAPANGWA KUNDI LA KIFO MECHI ZA KUFUZU AFCON.

SHIRIKISHO la Soka la Afrika CAF limepanga ratiba ya mechi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017 ambayo imezijumuisha nchi za Morocco na Tunisia. Morocco walikuwa wamefungiwa kushiriki fainali mbili za michuano hiyo kwa kukataa kuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka huu lakini adhabu ilitenguliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS baada ya kushinda rufani yao. Tunisia wao waliepuka adhabu adhabu baada ya kuomba adhi CAF kwa kuwatuhumu kuwa na upendeleo. Morocco wao wako katika kundi F sambamba na nchi za Cape Verde, Libya na Sao Tome huku Tunisia wao wakipambana na Togo, Liberia na Djibout katika kundi A. Katika ratiba hiyo kundi G ndio linalotabiriwa kuwa gumu zaidi kutokana na kuwajumuisha mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2013 Nigeria na Misri ambazo kila moja zitakuwa zikitaka kuepuka kushindwa kufuzu huku zingine zikiwa Tanzania na Chad.

Ratiba kamili ya mechi hizo ni:
KUNDI A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti
KUNDI B: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Angola, Afrika ya Kati, Madagascar
KUNDI C: Mali, Guinea ya Ikweta, Benin, Sudan Kusini
KUNDI D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoro
KUNDI E: Zambia, Congo, Kenya, Guinea Bissau
KUNDI F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome
KUNDI G: Nigeria, Misri, Tanzania, Chad
KUNDI H: Ghana, Mozambique, Rwanda, Mauritius
KUNDI I: Ivory Coast, Sudan, Sierra Leone, Gabon

No comments:

Post a Comment