MENEJA wa klabu ya Borussia Dortmund Jurgen Klopp anadhani Bayern Munich walistahili ushindi wa bao 1-0 waliopta katika mchezo dhidi yao jana. Klopp alishuhudia mchezo huo ambao mshambuliaji wa zamani wa kikosi chake Robert Lewandowski akifunga bao pekee katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Signal Iduna Park. Akihojiwa Klopp amesema dakika 10 za kwanza za mchezo zilikuwa nzuri lakini baada ya hapo hali haikuwa nzuri kwani walitengeneza nafasi chache za kufunga. Kocha huyo aliendelea kwa kukiri Bayern walicheza vyema zaidi hivyo walistahili ushindi huo ambao utawaweka katika nafasi ya nzuri ya kutetea taji lao la Bundesliga.

No comments:
Post a Comment