BASI la klabu ya Fenerbahce ya Uturuki limeshambuliwa kwa risasi na mtu aliyekuwa na siala baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo dhidi ya Rizespor ambao walishinda kwa mabao 5-1 jana. Dereva wa basi hilo alikimbizwa hospitali lakini hakuna mchezaji aliyepata majeraha yeyote katika tukio hilo ambalo lilitokea wakati wakisafiri kuelekea uwanja wa ndege wa Trabzon. Waziri mkuu wan chi hiyo Ahmet Dovutoglu ameamuru kufanyika uchunguzi wa haraka ili kubaini aliyefanya tukio hilo. Shirikisho la Soka la nchi hiyo limelaani vikali tukio hilo na katibu mkuu wa klabu Mahmut Uslu yeye akidai kuwa tukio la aibu katika soka. Uslu amesema walikwenda huko kufanya michezo na kucheza soka na sio vinginevyo.

No comments:
Post a Comment