MENEJA wa klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri anadhani wapinzani wao katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Monaco ni hatari zaidi kuliko Borussia Dortmund waliowatoa katika hatua ya mtoano. Kocha amekuwa akishuhudia msimu mzuri kwa timu yake kwani ikiwa imebaki miezi miwili kabla ya msimu kumalizika bado wako katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao la Serie A. Hata hivyo Juventus haijakuwa katika kampeni nzuri za michuano ya Ulaya katika misimu iliyopita lakini mwaka huu wana kubadili hilo kama wakifanikiwa kuwaondosha Monaco ambao hawapewi nafasi kubwa na kutinga hatua ya nusu fainali. Akihojiwa Allegri amesema ameishuhudia Monaco kidogo katika mchezo wao wa juzi dhidi ya Saint-Etienne na kuona kuwa wanaweza kuwa hawana ubora kama wa Dortmund lakini ni timu ngumu kucheza nayo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mchezo baina yao utakuwa kutokana na kutopewa kwao nafasi hivyo hawatakuwa na cha kupoteza.

No comments:
Post a Comment