NGULI wa Brazil Ronaldo de Lima amedai kuwa atatumia hata fedha zake mwenyewe kwa ajili ya kumchukua Lionel Messi kutoka Barcelona kwenda kuichezea klabu ya Fort Lauderdale. Messi amekuwa aking’ara La Liga kwa zaidi ya muongo mmoja na toka kuanza kwa mwaka huu amekuwa katika kiwango bora na kukisaidia kikosi chake kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi. Ronaldo ambaye aliwahi kuzichezea Barcelona na Real Madrid enzi zake hivi sasa ni mmiliki mwenza kwa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili na kubainisha nia yake ya kumuondoa Messi Camp Nou kwa fedha zake mwenyewe. Akizungumza katika uzinduzi wa msimu mpya wa ligi hiyo, Ronaldo amesema mbali na Messi lakini pia ana matumaini ya hata kumleta Cristiano Ronaldo aje aichezee timu hiyo. Ronaldo mbali na kumiliki klabu hiyo lakini pia ndio mshambuliaji wao kwasasa wakati wakijaribu kuipandisha timu katika Ligi Kuu ya Marekani-MLS.

No comments:
Post a Comment