MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anaamini kuwa taji la Ligi Kuu bado halipo ndani ya uwezo wao pamoja na kiwango bora wanachoendelea nacho hivi sasa. Ushindi wa mabao 4-1 waliopata dhidi ya Liverpool jana unaifanya timu hiyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu moja kwa moja michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya bila kucheza hatua za awali. Vinara Chelsea bado wameendelea kuondoza kwa tofauti ya alama saba juu yao, lakini Arsenal ambao wameshinda mechi 10 kati ya 11 walizocheza wana naafsi ya kupunguza pengo hilo wakati watakapoikaribisha Chelsea baadae mwezi huu. Pamoja na kiwango bora walichonacho, Wenger anaamini bado wana kazi kubwa ya kufanya kutokana na kuanza vibaya msimu. Wenger amesema kimahesabu wanaweza kushinda taji hilo lakini wanahitajika kuwa bora na wakati huohuo Chelsea kushuka kiwango jambo ambalo hadhani kama linawezekana.

No comments:
Post a Comment