MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesema timu yake imetumiwa meseji nyingi za kunyanyapaliwa katika mitandao ya kijamii kwasababu ya kuchoshwa. Kundi linalopinga meseji hizo limedai kuwa zaidi ya meseji 130,000 zilizotumwa kuhusiana na Ligi Kuu msimu huu, Chelsea ndio waliopata meseji nyingi zaidi kuliko klabu yeyote. Akihojiwa Mourinho ambaye timu yake inaongoza ligi kwa tofauti ya alama saba amesema anadhani wamepata meseji nyingi kwasababu watu wamechoshwa nao. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wamekuwa wakiongoza ligi toka mwanzoni mwa msimu mpaka sasa na hilo ndio jambo ambalo watu hawalipendi nchini humo.
No comments:
Post a Comment