MENEJA wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund, Ottmar Hitzfeld anaamini Jurgen Klopp anaweza kufuata nyayo zake na kwenda kuinoa Bayern Munich baada ya kuondoka Borussia Dortmund. Klopp alitangaza juzi kuwa amefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake katika majira ya kiangazi baada ya kuifundisha Dortmund kwa miaka saba na kuisaidia kunyakuwa mataji mawili ya Bundesliga na kutifa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Vilabu kadhaa vimeripotiwa kutaka huduma ya Klopp mwenye umri wa miaka 47 lakini Hitzfeld ambaye aliwahi kuinoa Dortmund kwa miaka sita na kasha kuhamia Bayern kwa misimu miwili anaamini kocha huyo anatakiwa kufikiria kwenda Allianz Arena kama kutakuwa na nafasi mwishoni mwa msimu huu. Hitzfeld amesema anajua kuwa Pep Guardiola bado ana mkataba na Bayern lakini anaweza kuamua kumpumzika mwishoni mwa msimu kama alivyofanya wakati akiwa na Barcelona. Kama hilo likitokea haoni sababu ya Klopp kushindwa kwenda kuinoa Bayern kwani vigezo vyote anavyo vya kuweza kuipa klabu hiyo mafanikio zaidi.
No comments:
Post a Comment