Thursday, April 16, 2015

PACQUIAO AANZA MAJIGAMBO.

BONDIA mahiri wa Ufilipino Manny Pacquiao ameanza majigambo akidai kuwa pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather litakalofanyika Mei 2 limekuja wakati muafaka baada ya kusubiriwa kwa kipindi kirefu. Mayweather mwenye umri wa miaka 38 na Pacquiao mwenye umri wa miaka 36 wanahesabiwa kuwa mabondia bora zaidi katika kizazi hiki na pambano lao linatarajiwa kuingiza kiasi cha paundi milioni 162. Pacquiao amesema ni jambo jema pambano hilo kufanyika hivi sasa kwani watu wengi wamekuwa na taarifa kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Pacquiao anashikilia mkanda wa dunia wa WBO na Mayweather mikanda ya WBC na WBA katika uzito wa welter na mikanda yote itapiganiwa katika pambano hilo.

No comments:

Post a Comment