VINARA wa Ligi Kuu ya Uturuki, Fernabahce wanatarajiwa kurejea uwanjani baadae leo baada ya kupumzika kwa wiki mbili kufuatia kushambuliwa kwa risasi kwa basi lao mapema mwezi huu. Fernabahce waligoma kucheza baada ya kushambuliwa Aprili 4 wakati wakitoka kucheza mchezo wa ligi na kupelekea ligi hiyo pia kusimamishwa kwa wiki moja kupisha uchunguzi. Klabu hiyo ilidai kuwa haitaweza kucheza mpaka suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi huku aliyehusika na kitendo hicho naye akitiwa mbaroni. Lakini ingawa uchunguzi wa kesi hiyo ukiwa bado unaendelea, mkurugenzi wa Fenabahce amesema wamekubali kucheza mchezo wa leo baada ya kuhakikishiwa usalama wao na serikali. Fenerbahce inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mersin katika mchezo wa maruadiano wa michuano ya Kombe la Uturuki huku wakiwa tayari wako mbele kwa mabao 2-1 waliyopata katika mchezo wa awali. Pia ligi ya nchi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho baada ya kusimamishwa.
No comments:
Post a Comment