KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Fabio Capello amedai kuwa nahodha wa Chelsea John Terry bado anastahili kuendelea kuichezea nchi hiyo. Capello aliyejiuzulu Februari mwaka 2012 baada ya Terry kuvuliwa unahodha na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kutokana na tuhuma za ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa QPR Antom Ferdinand. Terry mwenye umri wa miaka 34 alikutwa na hatia baada ya kesi yake kusikilizwa Julai mwaka 2012 lakini alifungiwa mechi nne na kutozwa faini ya paundi 220,000 na FA. Akihojiwa Capello amesema ni bora kuwa na mchezaji kama Terry katika kikosi cha Uingereza kwani bado ni mmoja ya wachezaji bora kabisa. Terry alistaafu soka la kimataifa Septemba mwaka 2012 baada ya kuitumikia Uingereza michezo 78 na kudai kuwa wakati wake wa kupisha vijana ulikuwa umefika.
No comments:
Post a Comment